Na Mwandishi Wetu
Katika kuhakikisha kuwa shughuli za udhibiti wa mbolea katika mipaka yote nchini zinafanyika kwa ufanisi zaidi, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA ) wamesaini hati ya Makubaliano ili kuimarisha ushirikiano.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti Bi. Happiness Mbelle amesema Makubaliano hayo baina ya taasisi hizi mbili yanalenga kuimarisha mawasiliano na kuongeza ufanisi katika shughuli za udhibiti wa mbolea mipakani.
Amesema kuwa kupitia mafunzo hayo shughuli za udhibiti wa mbolea zitaimarika zaidi hususan katika maeneo ya mipakani, baada ya maafisa hao kuelewa ipasavyo sheria ya mbolea , kanuni na taratibu mbalimbali za udhibiti.
Amesema maafisa hao wanaofanya kazi mipakani wanatarajiwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa katika maeneo ya ukaguzi na kushughulikia kwa makini nyaraka husika za uingizaji na usafirishaji wa mbolea nje ya nchi .
Pamoja na hayo Mada mbalimbali zilifundishwa ikiwemo majukumu ya TFRA, sifa za mkaguzi wa mbolea, maadili ya mkaguzi wa mbolea, nguvu ya kisheria aliyopewa mkaguzi wa mbolea na miongozo ya utekelezaji ukaguzi wa mbolea katika mazingira mbalimbali.
Awali akielezea lengo kuu la mafunzo hayo Meneja TFRA kanda ya Kaskazini Gothard Liampawe amesema wamelenga kuwajengea uwezo maafisa wa TPHPA waliopo mipakani ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi hususani katika kuimarisha ukaguzi wa mbolea zinazoingia na kutoka nchini na utoaji wa vibali kwa kuzingatia Sheria ya mbolea na 9 ya mwaka 2009, Kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.
Mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa na TFRA Kanda ya Kaskazini jijini Arusha ambapo maafisa wa TPHPA na TFRA wanaotoka mipakani walishiriki mafunzo hayo, yaliyoendeshwa na Meneja wa kanda ya Kaskazini Gothard Liampawe
Maafisa kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA ) wakiwa kwenye mafunzo ya pamoja ya kujengewa uwezo kuhusu uimarishaji wa udhibiti wa mbolea katika mipaka ikiwemo ukaguzi na kujua sheria ya mbolea, kanuni zake na taratibu za kushughulikia nyaraka mbalimbali za uingizaji na usafirishaji wa mbolea nje na ndani ya nchiMkurugenzi wa Huduma za udhibiti wa TFRA Bi. Happiness Mbelle akifungua mafunzo ya siku mbili kwa maafisa wa TPHPA na TFRA yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kufanya shughuli za udhibiti wa mbolea katika mipaka mbalimbali nchini.