Mwandishi Wetu,
Katika kutekeleza jukumu lake la kisheria,Mamlaka ya Udhibitii wa Mbolea Tanzania (TFRA) imefanya mapitio ya bei elekezi kwa aina kumi na saba (17) za mbolea ambapo aina nane (8) ni mbolea zinazoingizwa kutoka nje ya nchi (DAP, UREA, CAN, SA, NPKs, MoP, NPK Tobacco na TSP) na aina tisa (9) ni mbolea zinazozalishwa ndani ya nchi na Kampuni ya Itracom (Fomi Otesha, Fomi Kuzia na Fomi Nenepesha) na Kampuni ya Minjingu (Minjingu Nafaka Plus, Minjingu Top Dressing, Minjingu Pamba, Minjingu Chai, Minjingu Coffee, na Minjingu Tobacco).
Bei elekezi hizo, zitaanza kutumika kuanzia tarehe 15 Novemba, 2024 (Bei zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Kilimo; www.kilimo.go.tz na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA); www.tfra.go.tz.
Lengo la kufanya mapitio na kutangaza bei elekezi ni kuhakikisha kuwa mbolea inauzwa kwa bei inayoendana na gharama halisi za soko.
Wafanyabiashara wa mbolea wanatakiwa kuuza mbolea hizo kwa bei elekezi au chini yake.