WAZIRI AWESO AWAFUNDA WATAALAMU SEKTA YA MAJI.

 __Awaagiza kwenda kumsaidia Rais Mhe. Samia kutimiza  dhamira ya kumtuma mama ndoo Kichwani._

Mwandishi Wetu,

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefungua mkutano uliowakutanisha wataalamu wa Utawala na Rasilimali watu, Maendeleo ya Jamii na Maafisa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Sekta ya Maji.

Mkutano huu umefanyika jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Aweso amewaagiza wataalamu hao kumsaidia  Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  kufanikisha dhamiria yake ya kumtuma mama ndoo ya maji kichwani kwa vitendo.

"Niwaombe tuifanye kazi, Makundi yetu haya tuliyokutana leo hapa ni ya kimkakati na muhimu sana kuhakikisha Wizara na Taasisi zetu zinafanikiwa, kazi hii tunaiweza hivyo twendeni tukamsaidie Mhe. Rais kutimiza dhamira yake ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani"  Mhe. Aweso  ameeleza.

Mhe. Aweso amaeongeza kuwa Taasisi yoyote ikitengeneza mazingira mazuri na wezeshi kwa watumishi kutekeleza majukumu yake itafanikiwa na akayataka makundi haya kuwekeza katika huduma kwa wateja ili uhusiano baina yao na Taasisi za Wizara ya Maji yawe bora. 

Kwa upande mwingine Mh.Aweso amewataka Maafisa Utawala wa Wizara ya Maji na Taasisi zake kujitofautisha na wengine kwa kuongeza bidiii katika kujielimisha na kufahamu miongozo mipya, Sheria, Kanuni na Taratibu ili waweze kuwaongoza watumishi wa Sekta.

Naye Naibu Katibu Mkuu Bi Agnes Meena amewahakikishia watumishi wa Sekta ya Maji kuwa Wizara itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa.

Mkutano wa wataalamu wa Utawala na Rasilimali watu, Maendeleo ya Jamii na Maafisa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma katika Sekta ya maji unaofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 14 -16/11/2024 na umebeba kauli mbiu isemayo Rasilimali watu ni chachu ya maendeleo endelevu katika Sekta ya maji.



Post a Comment

Previous Post Next Post