Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele (wapili kulia) na Mjumbe wa Tume, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar wakishuhudia ufunguzi wa kituo cha kupigia kura No 1 katika Skuli ya Sebleni Jimbo la Kwahani Mkoa wa Mjini Mgaharibi leo tarehe 08 Juni,2024 ambapo wananchi wa jimbo hilo wanapiga kura katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo kumchagua Mbunge wao.
Wananchi wa jimbo la Kwahani wakihakiki majina yao kabla ya kwenda kupiga kura.
Msimsmizi wa Kituo No. 1 Shehiya ya Sebleni kilichopo katika Skuli ya Sebleni akifunga sanduku la kura kabla ya kuzanza zoezi la Uchaguzi.
Mpiga Kura akiandaliwa karatasi ya Kura tayari kwa Kupiga Kura
Mkazi wa Shehiya ya Sebleni akipiga Kura leo Juni 8, 2024 kumchagua Mbunge wa Jimbo hilo.
Wapiga Kura wakiwa katika mstari katika moja ya vituo vya Kupiga Kura Jimbo la Kwahani.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele ameshuhudia wananchi wa Jimbo la Kwahani Mkoa wa Mjini Magharibi wakipiga kura katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo kumchagua Mbunge wao.
Jaji Mwambegele aliambatana na Mjumbe wa Tume hiyo, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar ambapo walitembelea vituo hivyo vya kupigia kura na kushuhudia ufunguaji wa vituo saa moja kamili asubuhi.
Akizungumza baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika Skuli ya Sebleni, Uwanja wa Negro na Kariakoo, Jaji Mwambegele alisema zoezi linakwenda vizuri na wao walishuhudia vituo vikifunguliwa kwa wakati na wananchi kupiga kura.
Aidha, amesema vyama vya siasa vimeweka mawakala wakutosha katika katika vituo vyote vya kupigia kura walivyotembelea.
“Tumeshuhudia ufunguzi wa vituo na upigaji kura, vituo vimefunguliwa kwa wakati na wananchi wamejitokeza kwa wingi kuja kutumia haki yao ya kupiga kura pia vyama vya siasa vimeweka mawakala wakutosha katika vituo hivyo,”alisema Jaji Mwambegele.
Jaji Mwambegele amesema wananchi wa Jimbo la Kwahani wameonesha mwitikio mkubwa kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Vyama 14 vimesimamisha wagombea katika Uchaguzi huo mdogo wa kiti cha Ubunge jimbo la Kwahani ambapo majina yao na vyama katika Mabano ni Bw. Bashir Yatabu Said (Demokrasia Makaini), Bi. Nuru Abdulla Shamte (DP), Bi. Mwanakombo Hamad Hassan (NLD), Bi. Zainab Maulid Abdallah (CCK), Bi. Tatu Omary Mungi (UPDP), Bw. Khamis Yussuuf Mussa (CCM) na Bi. Jarade Ased Khamis (AAFP).
Wengine ni Bw. Kombo Ali Juma (NRA), Bi. Shara Amran Khamis (ADC), Bi. Naima Salum Hamad (UDP), Bi. Madina Mwalim Hamad (ADA TADEA), Bw. Amour Haji Ali (SAU), Bi. Mashavu Alawi Haji (UMD) na Bw. Abdi Khamis Ramadhan (CUF).
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akisalimia mawakala wa vyama waliokua katika Kituo cha Kupigia Kura.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele na Mjumbe wa Tume, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar wakiangalia vituo vya wazi vya kupigia kura
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akiangalia vituo vya wazi vya kupigia kura
Karani Muongozaji akihakiki jina la Mpiga Kura kabla ya kumruhusu kwenda Kupiga Kura.
Waangalizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kwahani wakishuhudia wananchi wa Jimbo la Kwahani wakipiga Kura leo.