STAMICO KINARA KUWAWEZESHA WATU WENYE UHITAJI MAALUMU

 

Mtendaji Mkuu wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse  (wapili kutoka kulia) akitembelea Banda la STAMICO Kwenye Maonesho ya Madini yanayoendelea katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.Mtendaji Mkuu wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse akizungumza na waandishi wa habari Juni 25, 2024 wakati alipotembelea banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Madini yanayoendelea katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma

…………..

Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) limedhamiria kuwawezesha watu wenye Ualbino pamoja na kikundi cha Wanawake na Samia ili kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi kwa kuwagawia Kontena na Uwakala wa Rafiki Briquettes ili wajiongezee kipato kwa ukizingatia wanawake ni jeshi kubwa hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Juni 25, 2024 wakati alipotembelea banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Madini yanayoendelea katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma, Mtendaji Mkuu wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse, amesema kuwa STAMICO ni Shirika la umma na moja ya jukumu lake kuu ni kuwekeza kwa niaba Serikali pamoja na kuwezesha makundi maalumu ili kunufaika na rasilimali za madini.

“STAMICO ni walezi wa Vikundi vya kina Mama na Samia tangu kuasisiwa kwake Mkoani Geita Vimewezeshwa na kuanzisha miradi ya kuuza nishati safi na salama ya Rafiki Briquettes na vikundi hivi vipo nchi nzima, lengo ni kuwezeshwa kiuchumi na jamii kunufaika na utunzaji wa Mazingira kwa kuacha kukata miti kwa ajili kutafuta kuni” amesema Dkt. Mwasse.

Aidha Dkt. Mwasse ameipongeza FEMATA kwa kuandaa maonesho ya Wiki ya Madini Dodoma ambapo wadau wengi wananufaika kupitia mafunzo na makongamano yanayoendelea.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya watu wenye Ulemavu (FDH) Bw. Maiko Salali, ameishukuru STAMICO kwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na dhana potofu na pamoja na kuwapatia Kontena ili waweze kuuza mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes.

Bw. Salali amesema kuwa kwa sasa watu wenye Ualbino sio omba omba tena kwani wamekuwa na utamaduni wa kutafuta fursa za kibiashara na kufanikiwa kuwezeshwa na STAMICO, huku akitoa wito kwa Mashirika mengine kuiga mfano wa shirika la madini.

Maonesho ya madini yanafika tamati 27 Juni, 2024 huku yakiwa yamebebwa na kaulimbiu isemayo : Amani iliyopo nchini inapaswa kuleta uchumi imara kupitia soko la madini la Afrika nchini Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post