.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe.George Simbachawene akizungumza na wakristo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei Mang’ola Chini wakati wa harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kubadilisha paa la Kanisa hilo lililopo Mang’ola Chini, Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha, ambalo limekuwa likivuja wakati wa mvua na hivyo kusababisha wakristo kushindwa kukaa ndani.
Sehemu ya Wakristo wa Parokia ya Mang’ola Chini wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora , Mhe.George Simbachawene wakati wa harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kubadilisha paa la Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei Mang’ola Chini, Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha, ambalo limekuwa likivuja wakati wa mvua na hivyo kusababisha wakristo kushindwa
Mhashamu Askofu wa Antony Lagwen wa Jimbo Kuu Katoliki Mbulu akizungumza na wakristo wa Parokia ya Mang’ola Chini wakati wa harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kubadilisha paa la Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei Mang’ola Chini, Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha, ambalo limekuwa likivuja wakati wa mvua na hivyo kusababisha wakristo kushindwa kukaa ndani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe.George Simbachawene akiwa na Mhashamu Askofu Antony Lwagen wakiwa pamoja na viongozi wengine akiangalia baadhi ya eneo la Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei Mang’ola Chini ambalo limekuwa likivuja wakati wa mvua na hivyo kusababisha wakristo kushindwa kukaa ndani.
Baadhi ya wanakwaya ya Mtakatifu Cecilia wakiingia kwa kuimba wakati wa misa takatifu iliyoendeshwa Mhashamu Askofu wa Antony Lagwen wa Jimbo Kuu Katoliki Mbulu kabla ya harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kubadilisha paa la Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei Mang’ola Chini, Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha, ambalo limekuwa likivuja wakati wa mvua na hivyo kusababisha wakristo kushindwa kukaa ndani
…….
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema mikopo ni moja ya vyanzo vya mapato ya serikali kote duniani, hivyo Tanzania kukopa siyo aibu wala kujidhalilisha, bali ni sifa njema kwa kuwa inakopesheka.
Simbachawene ametoa kauli wakati akizungumza kwenye harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kubadilisha paa la Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu,Yuda Tadei Mang’ola Chini, Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha, ambalo limekuwa likivuja wakati wa mvua na hivyo kusababisha wakristo kushindwa kukaa ndani.
Amesema vyanzo vya mapato vya Kanisa ni pamoja na sadaka ya kila jumapili, zaka, misaada mbalimbali pamoja na harambee huku akitaja vyanzo vya mapato vya Serikali kuwa ni kodi, tozo, misaada na mkopo, na kusema kukopa ni moja ya chanzo cha mapato ya serikali na serikali zote duniani zinakopa.
Aidha amesema kama ingetokea Tanzania haiwezi kukopesheka hiyo ndo ingekuwa aibu lakini kwa kuwa inakopsheka hiyo ni heshima kubwa kwa watanzania kwa kuwa inakopa ili kutekeleza miradi ya maendeleo na kama isipofanya hivyo itapelekea nchi kupata madhara makubwa ambayo yasingetokea kama ingekopa.
Amesema Nchi zote duniani ikiwemo Marekani na China zinakopa na zinadaiwa na kwamba kodi inayokusanywa nchini haina uwezo wa kutekeleza miradi hiyo na kama kodi hiyo itaweza kutumika inaweza kuchukua zaidi ya miaka 40 ili kukamilisha miradi hiyo.
“Vyanzo vya mapato vya Kanisa ni sadaka ya kila jumapili, zaka, misaada mbalimbali pamoja na harambee ambapo harambee ni hatua ya mwisho ya utafutaji wa fedha kwa Taasisi za dini, lakini vyanzo vya mapato vya Serikali ni kodi, tozo, misaada na mkopo, hivyo kukopa ni moja ya chanzo cha mapato ya serikali na serikali zote duniani zinakopa”amesema Simbachawene na kuongeza kuwa
“Kukopa ni chanzo cha mapato hivyo isionekane Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inapokwenda kutafuta mkopo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo ndo inakopa sana”.
Amesema kutokana na mahitaji makubwa ya nchi suala la kukopa haliepukiki akitolea mfano uendelezaji wa Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere ambalo gharama yake ni zaidi ya trioni 6 huku bajeti ya Serikali ya mwaka mzima ikiwa ni tirioni 43 huku zaidi ya asilimia 7O ya fedha hizo zikitumika kwa ajili ya uendeshaji wa nchi na asilimia 30 ndizo hupelekwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo
“Hivi tungetaka kujenga reli ya SGR kwa kodi yetu tungejenga kwa miaka mingapi?amehoji Simbachawene na kusema ikijengwa kwa miaka 100 itakuwa na tija kweli na tukiamua tutaweza kujenga kwa miaka 50 au 60 ambapo hapo tutaacha kulipana mishahara, kusomesha watoto pamoja na kutibu wagonjwa “