REA YATENGA SHILINGI BILIONI 3 KUTOA RUZUKU MRADI WA USAMBAZAJI MITUNGI YA GESI YA KUPIKIA

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini-REA imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3 kwaajili ya kutoa ruzuku katika mradi wa Usambazaji wa mitungi ya Gesi ya kupikia wenye uzito wa kilogramu sita.

Ameyasema hayo leo Mei 3, 2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Masoko na Teknolojia-REA, Mhandisi Advera Mwijage wakati wa kikao cha kutoa mwongozo kwa waombaji wa ruzuku ya kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia.

Amesema katika mradi huo wa majaribio, REA inakusudia kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia takribani laki moja katika mikoa ya Tanzania bara.

"Kwa mantiki hiyo kila Mkoa utakuwa na wastani wa Mitungi elfu nne itakayogawiwa bure kwa wananchi hasa vijijini". Amesema

Aidha amesema kwa mwaka zaidi ya hekari laki nne za miti hukatwa na wananchi kwa matumizi ya kuni na mkaa, hivyo uwepo wa mradi wa kutoa ruzuku ya mitungi ya gesi bure kwa wananchi kutasaidia kuondokana na changamoto ya ukataji wa miti.

Hata hivyo, Mhandisi Advera amewataka wasambazaji wa mitungi ya gesi ya kupikia kuelewa kuwa wawe makini na walete mitungi ya gesi iliyo na ubora la sivyo Serikali haitasita kuvunja mkatana na Wakala wa Usambazaji.

Pamoja na hayo amesema Serikali imekusudia kuboresha maisha ya mwananchi kwa kuona anatumia nishati bora ya kupikia ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Masoko na Teknolojia-REA, Mhandisi Advera Mwijage akizungumza katika kikao cha kutoa mwongozo kwa waombaji wa ruzuku ya kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia kilichofanyika leo Mei 3,2023 Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Masoko na Teknolojia-REA, Mhandisi Advera Mwijage akizungumza katika kikao cha kutoa mwongozo kwa waombaji wa ruzuku ya kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia kilichofanyika leo Mei 3,2023 Jijini Dar es Salaam.

 Wadau mbalimbali wa Gesi za kupikia wakiwa katika kikao cha kutoa mwongozo kwa waombaji wa ruzuku ya kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia majumbani kilichofanyika leo Mei 3,2023 Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post