DAWASA YASHIRIKI MATEMBEZI KWA AJILI YA KUONA UHALISIA WA UPATIKANAJI WA MAJI

 Katika kusherekea maadhimisho ya wiki ya maji Duniani yaliyoanza tarehe 16 hadi Machi 22 mwaka 2023, Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ukishirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) leo Machi 19, 2023 wamefanya matembezi kwa ajili ya kuona uhalisia ni kwanamna gani wananchi hasa vijijini wanavyotumia muda mwingi na mwendo mrefu kutafuta maji safi na salama. Matembezi hayo yameanzia makao makao makuu ya Vodacom mpaka Makumbusho ya Taifa, Posta Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza mara baada ya kumaliza matembezi hayo ya zaidi ya kilometa 10, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael Battle amesema matembezi haya ni Kwa ajili ya kupata uhalisia wa namna wananchi hasa wa vijijini wanavyopata tabu ya kutembea mwendo mrefu kwa ajili ya kutafuta maji.

Pia amesema Ubalozi wa Marekani utaweza kuongeza nguvu kwenye Serikali ya Tanzania kwa kuweza kuanzisha miradi mbalimbali ya Maji ili kuondoa hadha ya upatikanaji wa maji hapa nchini hasa vijijini.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema inakadiriwa watu bilioni 4 Duniani kote wanakosa maji safi na salama na asilimia 54 ya watu wote duniani wanachangamoto ya usafi wa mazingira.

Pia amemshukuru Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle kwa kuweza kuandaa matembezi haya ikiwa ni kuunga jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ameweka nguvu nyingi hasa kuanzisha miradi mbalimbali ya Maji ili kuweza kumtua ndoo mama kichwani.

"Serikali kupitia wizara ya maji iko kwenye wiki ya maadhimisho ya maji Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni Kuongeza Kasi ya Mabadiliko katika sekta ya maji kwa Maendeleo endelevu ya uchumi hivyo kama Serikali tumejipanga kuweza kuongeza wigo wa upatikani wa maji hapa nchini hasa vijijini. Alisema Mhandisi Luhemeja 

Pia Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Kiula Kingu amewashukuru wadau wote walioshiriki kwenye matembezi hayo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kwa kuweza kuamua kuonesha uhalisia wa namna watu hasa wa vijijini wanavyopata tabu kwenye kupata maji safi na salama ambao wako nje ya mtandao wa maji.

Amesema DAWASA inaendela na maadhimisho ya wiki ya maji Duniani kwa kutoa elemu hasa ya utunzaji wa vyanzo vya kuvituza ili na sisi kututunza.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Kiula Kingu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) pamoja na washiriki wengine mara baada ya kumaliza matembezi kwa ajili ya kuonesha uhalisia wa namna wananchi wanayotembea umbali mrefu kutafuta maji iliyoandaliwa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kwa kushirikiana na DAWASA.

Post a Comment

Previous Post Next Post