KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA MABANDA YALIOSHIRIKI KUONESHA BIDHAA ZAO NCHINI AFRIKA KUSINI

 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi leo Machi 16, 2023 ametembelea mabanda mbalimbali kutoka Tanzania na Afrika ya Kusini yaliyoshiriki kuonesha bidhaa zao na huduma kwenye Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation) kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

Mkutano huo umehitimishwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa

Maonesho hayo yalifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Afrika ya Kusini (CSIR ICC) mjini Pretoria.






Post a Comment

Previous Post Next Post