MAAFISA HABARI SERIKALINI KUONGEZA NGUVU KUISHANGILIA TAIFA STARS







Eleuteri Mangi-WUSM, Dar es salaam

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali wanaoshiriki kikao kazi cha 18 cha Mwaka 2023 jijini Dar es Salaam wamepewa tiketi kwenda kuishangilia Timu ya Taifa, Taifa Stars ambayo inaotarajia kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Timu ya Taifa ya Uganda, Uganda the Cranes utakachezwa Machi 28, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu amewahimiza washiriki wa kikao kazi hicho kutumie fursa hiyo ambayo imetolewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kutoa tiketi
takriban 600 pamoja na usafiri kwa  washiriki wote kwenda uwanjani na kurudi kuongeza hamasha kwa Timu Taifa Stars katika mchezo huo muhimu ili kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2024 nchini Ivory Coast.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Saidi Yakubu, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Mkomi na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi ni miongoni mwa Makatibu ambao wameshiriki ufunguzi wa kikao kazi hicho.

Post a Comment

Previous Post Next Post