TANAPA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA HIFADHI YA TAIFA KILIMANJARO MACHI 16,MWAKA HUU


Naibu kamishna wa uhifadhi na maendeleo ya biashara, Herman Batiho akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha ,aliyepo pembeni yake ni Kamishna msaidizi  wa uhifadhi ambaye pia ni Mkuu wa hifadhi ya Taifa Kilimanjaro,Anjela Nyaki .
******************
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.SHIRIKA la Hifadhi za Taifa TANAPA,linatarajia kufanya maadhimisho ya kwanza ya  miaka 50 tangia kuanzishwa kwa hifadhi ya Taifa  Kilimanjaro yatakayofanyika, Machi 16 Mwaka huu katika makao makuu ya mlima huo yaliyopo, Marangu Mkoani Kilimanjaro .
Akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha,Naibu Kamishna wa Uhifadhi na maendeleo ya biashara,Herman Batiho  amesema maadhimisho hayo  ya kwanza ya aina yake , yanalenga pia kuutambulisha umma kuwa mlima huo  unapatikana katika nchi pekee ya Tanzania.
Amesema kuwa, kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Marangu, mkoani Kilimanjaro, huku Makamu wa Rais dkt Philip Mpango akitarajiwa kuwa mgeni Rasmi. 
Amesema maadhimisho ya  jubilee ya miaka 50 ya mlima Kilimanjaro ni utaratibu wa kawaida wa Tanapa na hii ni baada ya kufanya maadhimisho kama hayo ya miaka 60 ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti. 
Kilele cha Mlima kilimanjaro kitafanyika Marangu Mkoani Kilimanjaro  yalipo makao makuu ya Mlima huo huku makamu wa rais dkt Philip Mpango akitarajiwa kuwa mgeni rasmi “amesema 
Amesema mlima huo wenye urefu wa kilometa 5,895 ulianzishwa rasmi kama hifadhi ya Taifa Kilimanjaro , Machi 16, Mwaka1973 kwa ajili ya shughuli za utalii. 
Naye kamishna  msaidizi wa  hifadhi,Angela Nyaki ,amesema kuwa maadhimisho hayo yataanza Machi 1,hadi kilele machi 16 mwaka huu,na mambo mbalimbali yatafanyika ikiwemo usafi wa Mlima utakaofanyika kwa siku kumi kuanzia machi 1,ambapo wadau wa utalii wapatao 500 watashiriki.
Amesema shughuli zingine zitakazofanyika katika sherehe za maadhimisho hayo  ni pamoja na ugawaji na upandaji wa miti, zoezi litakalozinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.
“Pia tutawatembelea waongoza utalii wa miaka ya 70 ili kuzungumza nao na kupata uzoefu wao na ushauri wao”amesema .
Amesema tangu kuanzishwa kwa shughuli za utalii katika mlima Kilimanjaro, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo ongezeko la watalii na kufikia elfu 50 kwa mwaka, kuongezeka kwa njia za kupandisha mlima huo kutoka njia moja hadi kufikia njia sita .

Post a Comment

Previous Post Next Post