BODI YA WAKURUGENZI TBS YAZIPONGEZA OFISI ZA TBS KANDA YA KASKAZINI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE IPASAVYO

 

 
BODI ya Wakurugenzi Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetembelea ofisi za Shirika hilo zilizopo kanda ya Kaskazini kuona kazi zinaendaje na kama kuna kitu cha kuboreshwa kiboreshwe ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabiri.
 
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof.Othuman Chande amesema kuwa watafanya kazi kwa nguvu moja lengo ni kuhakikisha wanasimamia sheria ya ubora wa bidhaa hasa kwenye maeneo ambayo bidhaa zinapita kwa wingi.
 
Amesema sehemu zote walizopita wamekuta kazi zinakwenda vizuri japokuwa kuna changamoto ndogondogo ambazo wameomba kuzishughulikia ili Shirika hilo liendelee kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora Bw.Lazaro Msasalaga amesema wamekuwa na  utaratibu wa kufuatilia bidhaa sokoni ziwe za kutoka nje au za kutoka ndani ya nchi ambapo wanapita kwenye masoko na maduka wanazinunua na kwenda kuzipima kujihakikishia kwamba kweli zinaendelea  kukidhi ubora na usalama.
 
“Mifumo yote inasimamia vizuri nashukuru wadau mbalibali wanatoa ushirikiano na tuendelee kuomba wadau wa kutosha kwasababu TBS haiwezi kuona kila kitu na kila mahali nchini kwahiyo wadau wengi wanatupatia taarifa za msingi na sisi tunakuwa tunazifuatilia na kuchukua hatua za kisheria”. Amesema 

Post a Comment

Previous Post Next Post