KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MRADI WA MAJI TINDE - SHELUI

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika Tenki la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Tinde Mkoani Shinyanga hadi Shelui mkoani Singida.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akizungumza Mkandarasi ambaye anatekeleza Mradi wa Majisafi na salama wa Ziwa Victoria kutoa Tinde hadi Shelui Arnab Saha kutoka Kampuni ya WAPCOS.


Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiwasili kukagua Tenki la Maji la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Tinde wilayani Shinyanga kwenda Shelui mkoani Singida.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika Tenki la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Tinde hadi Shelui.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika Tenki la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Tinde hadi Shelui.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika Tenki la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Tinde hadi Shelui.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika Tenki la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Tinde hadi Shelui.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika Tenki la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Tinde hadi Shelui

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KATIBU Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga, ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa maji safi na salama ya Ziwa Victoria kutoka Tinde wilayani Shinyanga hadi Shelui mkoani Singida.

Amebainisha hayo leo Januari 4, 2022 wakati alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo katika Mji wa Shelui na Tinde wilayani Shinyanga.

Amesema mradi huo wa maji ya Ziwa Victoria ambao unatoka Tinde kwenda Shelui mkoani Singida umekamilika kwa asilimia 99, na tayari wananchi wa Shelui wameanza kutumia maji.Kwa upande wa Tinde kinachosubiliwa ni usambazaji na ulazaji wa mabomba.

“Mradi huu wa Maji wa Tinde mkoani Shinyanga hadi Shelui mkoani Singida umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 24.6 na umekamilika kwa asilimia 99 tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha, ili wananchi wake wapate huduma ya majisafi na salama,” amesema Mhandisi Sanga.

Aidha, amewasihi watumishi wa Wizara pamoja na Mamlaka za Maji waendelee kutunza miundombinu hiyo ya maji pamoja kutunza Mazingira, ili mradi huo uwe endelevu na kuwahudumia wananchi kwa muda mrefu.

Kwa upande Mhandisi wa Mipango na Ujenzi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (SHUWASA) Wilfred Lameck, amesema mradi huo wa Maji kwa upande wa Shinyanga utahudumia wakazi wa Tinde na Didia wapatao elfu 18, na sasa wanasubiri zoezi la ulazaji wa bomba za usambazaji maji kuanza kufanyika ili huduma ianze kutumika.

Post a Comment

Previous Post Next Post