TANESCO YAPAMBANA KUMALIZA UPUNGUFU WA UMEME


 SHIRIKA la umeme nchini(TANESCO),limesema wa kipindi kifupi wamefanya jitihada za kupunguza makali ya mgao wa umeme kwa kufanya marekebisho ya mitambo mmoja ubungo na kusaidia kuingiza megawati 35 katika gridi ya taifa na mtambo mmoja wa kituo cha kinyerezi namba 2 yamekamilika na kuzalisha megawati 215 za umeme.

Pia,Tanesco imesema imeshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha kidatu na kuanza kuzalisha megawati 50 za umeme katika gridi ya Taifa kuanzia novembe 24 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na mkurugenzi mkuu wa TANESCO,Maharage Chande,wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya kuhusu Jitiha zinazofanyika na shirika hilo kukabiliana na upungufu wa umeme,

Amesema kutokana na matengenezo hayo kukamilika imepelekea kupungua wastani ya kati ya megawati 300 hadi 350 wiki iliyopita hadi kufikia megawati 215 za umeme wiki hii

Aidha,Chande,amesema mvua zilizonyesha maeneo mbalimbali nchini hazaweza kujaza kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ya Pangani na Kihansi na kupelekea kuendelea kuwepo kwa upungufu wa umeme kwenye gridi ya taifa.

Hata hivyo,Chande,amesema iwapo mvua zitaendelea kunyesha katika mabwawa yote ya kufua umeme na matengenezo yaliobaki kukamilika kama yalivyopangwa yatasaidia kumalizika mgao wa umeme.

Post a Comment

Previous Post Next Post