BRELA YAPATA TUZO YA TPSF





 


Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zilizotambuliwa  na  Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) katika siku ya TPSF, kutokana na mchango wake katika kukuza uwekezaji  wa sekta binafsi nchini.  

Hafla hiyo imefunguliwa rasmi na  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, tarehe 02 Novemba 2022. katika ukumbi wa The SuperDome Arena) Masaki, Jijini Dar es salaam.

Katika hafla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa  BRELA, Bw. Gofrey Nyaisa amekabidhiwa  tuzo  hiyo na Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji,  BRELA ikiwa ni miongoni mwa Taasisi za Umma kadhaa zinazochangia katika ukuaji wa sekta binafsi na uchumi wa nchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post