MATUKIO KATIKA PICHA MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIANCHI

 


Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa akiwasilisha Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2023) kwa wadau na wageni mbalimbali waliotembelea banda la maonesho la Tanzania katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri.

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba akitoa ufafanuzi baada ya Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2023) kuwasilishwa kwa wadau na wageni mbalimbali waliotembelea banda la maonesho la Tanzania katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama akisalimiana na Bw. Edwado Freitas Meneja wa Kanda ya Afrika wa Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi. Kikao baina yao kimefanyika katika banda la maonesho la Tanzania katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri

Picha ikionesha mawasilisho mbalimbali yakiendelea katika banda la Tanzania katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri. Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Nishati na Taasisi zake, Wizara ya Maliasili na Utalii na Benki ya CRDB zinashiriki katika maonesho hayo.

Rais wa Total Energy Duniani Bw. Patrick Pouyanné akizungumza na ujumbe wa Tanzania katika maonesho yanayoendelea katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri alipotembelea banda la maonesho la Tanzania.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).

Post a Comment

Previous Post Next Post