*HUDUMA YA VISIMA VIREFU*
Kazi ya kufufua kisima cha maji eneo la Kimani, kata ya Pugu Wilaya ya Ilala chenye urefu wa mita 90 imeanza ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa *Kimani, Dunda, Pugu Bombani, Pugu kwa Rais, Kinyamwezi, Buyuni, Taliani na Mgeule.*
Kisima kina uwezo wa kuzalisha maji lita *1,440,000* kwa siku
Visima hivi vitapunguza changamoto ya upungufu wa maji iliyopo sasa, DAWASA ina jumla ya visima 160 vilivyo katika mfumk na vinavyozalisha lita milioni 26.9. Kwa kukamilika kisima hiki, jumla ya visima katika mfumo vitakuwa 161 na uwezo wa uzalishaji kwa siku utafikia lita milioni 28.34