WAZIRI BALOZI DKT CHANA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA, MSUMBIJI



                                  ………………………

Na Sixmund Begashe NMRT

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana leo Agosti 4, 2022 ameshiriki Mkutano wa kwanza wa Kikanda kuhusu Usimamizi Endelevu wa Misitu ya Miombo Jijini Maputo nchini Msumbiji.

Mkutano huo unahudhuriwa na viongozi wa juu wa Kisekta kujadili umuhimu ya uhifadhi wa misitu ya miombo huku msisitizo ukitolewa kwa nchi zote za Afrika kuhakikisha zinaongeza nguvu katika kuhifadhi rasilimali hiyo muhimu kwa maisha ya Waafrika na Dunia kwa Ujumla.

Katika Mkutano huo wa Kimatifa, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameambatana na Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo.

Post a Comment

Previous Post Next Post