BoT YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI JIJINI MBEYA

 


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson, akisalimiana na Mkurugenzi wa Tawi la BoT Mbeya, Bw. Ibrahim Malogoi, alipofika mapema leo katika banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.  

Kaimu Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Victoria Msina akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson, zawadi ya pochi ambazo pia hutumika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji sahihi wa noti. 

 Mhasibu Mkuu Mwandamizi BoT, Bw. Elirehema Msemembo akitoa elimu kuhusu Alama za Usalama za Noti zetu kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya. Kulia kwake ni Meneja Msaidizi Idara ya Sarafu, Bw. Nixon Kyando

Afisa Utawala Mwandamizi BoT, Bw. Dennis Alfred, akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. 

Wachambuzi wa Masuala ya Fedha, Bw. Hassan Mbaga na Bi. Laila Kisombe wakitoa elimu kuhusu namna ya kuwekeza katika dhamana za serikali kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.  

Afisa Mkuu Mwandamizi wa Benki, Bi. Joyce Njau, akielezea namna BoT inasimamia mifumo ya malipo nchini kwa wananchi waliotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Post a Comment

Previous Post Next Post