BoT YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

 

Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji BoT, Bw. Kened Nyoni na Mkurugenzi wa Tawi la BoT Mbeya, Bw. Ibrahim Malogoi, wakijadiliana jambo na Afisa Mkuu Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma BoT, Bw. Lwaga Mwambande, katika banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Katikati ni Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina. 

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Sebastian Waryoba, akizungumza na Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina, alipotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya.  

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Sebastian Waryoba, akipewa maelezo na Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi BoT, Bi. Consolata Shao, kuhusu Kurugenzi ya Utumishi na Uendeshaji alipotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya.  

Mkaguzi wa Mabenki Mwandamizi, Bw. Gwamaka Charles, akielezea jambo kuhusu namna BoT inasimamia sekta ya fedha nchini kwa mwananchi alietembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya.  

Meneja Msaidizi Masomo ya Muda Mfupi, Chuo cha BoT, Bi. Tulla Mwigune, akifafanua jambo kuhusu Chuo cha BoT kwa mwananchi alietembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya. 

Post a Comment

Previous Post Next Post