TFRA YAANDAA MFUMO RAFIKI NA RAHISI WA UPATIKANAJI WA MBOLEA KWA WAKULIMA

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt. Stephan Ngailo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) katika mkutano maalum na waandishi hao kuelezea hali ya upatikanaji wa mbolea kwa wakulima. Mkutano huo umefanyika leo Ogasti 2-2022 katika Banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya. (katikati) ni Kaimu Meneja Uhusiano, Mawasiliano na Elimu kwa Umma Matilda Kasanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt. Stephan Ngailo (wa nne kulia) akiwa pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo katika mkutano huo.

Sehemu ya waandishi wa habari walikuwa katika mkutano huo wakimsikiliza Mkurugenzi wa TFRA Dkt. Stephan Ngailo mapema leo Agosti 2,2022 Katika Banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.

Wauzaji wa mbolea Penina Mwita ( kulia mwenye fulana ya rangi ya pinki) na Leonald Mpayo (wa pili kulia) wakimuhudumia mteja aliyefika kwenye Banda lao katika maonesho hayo.

………………………………………….

Katika kuhakikisha wakulima wote wanafikiwa na huduma ya upatikanaji wa mbolea ya ruzuku, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesema kuwa imeandaa mfumo rafiki utakaowawezesha wakulima kushiriki katika mnyororo wa mbolea ya ruzuku ikiwa na lengo kufanya wananchi wapate mbolea hiyo bila vikwazo .
Hayo yamesemwa leo Agosti 2.2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa  Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dk.Stephan Ngailo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katka Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Dkt. Ngailo amesema kuwa katika mnyororo wa mbolea ya Ruzuku wadau  wote wanatakiwa kujisajili katika mfumo ili kuondoa changamoto ya kumfikia mkulima wakati wa msimu wa kilimo unapoanza ambapo wadau hao wanaotakiwa kujisajili katika mfumo waagizaji  wa mbolea kutoka nje ya nchi , Wazalishaji wa Mbolea nchini , Mawakala wa Mbolea nchini pamoja na wakulima ambao ndio walengwa wa mbolea ya ruzuku.
Dk.Ngailo amesema kuwa kwa upande wa wakulima watajisajili katika ofisi za kijiji ambao watapewa namba maalum ambapo atapokwenda kwa wakala ataonesha na kununua mbolea kwa bei nafuu.
Amesema serikali imefanya hivyo katika kuwa na usalama wa chakula pamoja na kuongeza uzalishaji  wa mazao nchini.
“TFRA imejipanga katika kusimammia mbolea ya ruzuku kwani Rais Samia Suluhu Hassan ametoa Ruzuku ya mbolea ili kuhakikisha wananchi wanapunguziwa makali ya kununua mbolea” amesema Dkt. Ngailo.

Aidha amesema katika maonesho ya Nane Nane Kitaifa

Post a Comment

Previous Post Next Post