WAZIRI BALOZI DKT. PINDI CHANA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA MRADI WA REGROW



                            ……………………..

Na Sixmund Begashe NMRT

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wizara yake fedha za utekelezaji wa Mradi wa kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Utalii Kusini mwa Tanzania( REGROW).

Mhe. Balozi Dkt Chana ametoa shukurani hizo Mkoani Njombe alipopewa nafasi na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan asalimie wananchi wa Kijiji Cha Halali Wilayani Wanging’ombe wakati wa mapokezi yake mkoani humo.

Licha ya kuelezea Mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ya Utalii kupitia kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii kupitia Filamu ya The Royal Tour, Waziri Balozi Dkt Chana amemshukuru kwa kutoa fedha Dola za Marekani milioni 150 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa REGROW ambao umekuwa msaada mkubwa katika kuendeleza sekta ya Utalii nchini.

Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Njombe

Post a Comment

Previous Post Next Post