TBS YAKUTANA NA WAZALISHAJI, WAINGIZAJI WA VILAINISHI VYA MAGARI HAPA NCHINI

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu (TBS), Bw.David Ndibalema (katikati) akiwa kwenye kikao cha waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu (TBS), Bw.David Ndibalema akizungumza kwenye kikao cha waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu (TBS), Bw.David Ndibalema akifungua kikao cha waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi udhibiti Ubora, Dkt. Candida Shirima akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini.  Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini wakiwa kwenye kikao na wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam.

 Waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini wakiwa kwenye kikao na wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam.

********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), inawajibika kikamilifu kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini na zile ambazo zinazoingizwa kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na biddhaa za vilainishi vya magari  zinakidhi matakwa ya viwango ili kukuza uchumi wa nchi.

Ameyasema hayo leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu (TBS), Bw.David Ndibalema wakati akifungua kikao cha waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini 

Amesema kuwa wameandaa mkutano huo mahususi kwa lengo la  kukuza uelewa ili kukidhi matakwa ya viwango kwa bidhaa za vilainishi vya magari hususan oili za injini za magari.

“Ni vyema kutambua kuwa ubora wa vilainishi vya magari ni muhimu katika kutunza vyombo hivyo, ikumbukwe kuwa endapo mtumiaji atanunua vilainishi visivyokidhi vigezo  vya ubora huweza kusababisha uharibifu wa gari na kutopata thamani ya fedha zilizotumika”. Amesema.

Amesema TBS itaendelea kutilia mkazo suala la usimamizi wa viwango na kudhibiti usalama na ubora wa bidhaa ili kuhakikisha zinakidhi vigezo vya usalama na ubora.

Post a Comment

Previous Post Next Post