WAZIRI AWESO AAGIZA KUONGEZWA NGUVU KAZI MRADI WA MAJI BUTIMBA


WAZIRI  wa Maji Jumaa Aweso (kushoto) akizungumza eneo la mradi wa maji Butimba leo,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele na katikati ni Meneja Ufundi wa Mradi huo kutoka kampuni ya SOGER SATON, Denis Mutegi.

Meneja Ufundi wa kampuni ya SOGER , Denis Mutegi (kushoto kwa kwanza) akimwongoza Waziri wa Maji, Jumaa Awesso leo  kukagua mradi huo. 

Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele, akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la mradi wa Maji Butimba wakati wa ziara ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, 

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na wafanyakazi wanaojenga mradi wa chanzo cha Maji Butimba leo.Picha zote  na Baltazar Mashaka 

…………………………………

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

WAZIRI wa Maji Juma Aweso amewatahadhari wakandarasi wasiokwenda na kasi ya utekeleleza wa miradi kulingana na mkataba wataachana nao na kuweka wengine watakaofanya kazi kwa wakati wananchi wapate maji, wakizingua watazinguana.

Pia amemwagiza mkandarasi wa mradi wa chanzo kipya cha Maji Butimba, kuongeza nguvu kazi ili ukamilike kwa wakati kulingana na viwango vya ubora na mkataba na kuwalipa wafanyakazi haki za jasho lao.

Waziri Awesso alitoa agizo hilo leo alipotembelea mradi huo akiwaongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mwanza (MWAUWASA) akiwemo Mkurugenzi Mtendaji na wataalamu wa mamlaka hiyo.

Alisema mradi huo kwa Wizara ya Maji ni wa kimkakati, unatakiwa kutatua changamoto ya maji katika maeneo mengi ya Jiji la Mwanza, hivyo MWAUWASA wausimamie kwa weledi na hatataka kusikia michakato na variation.

 “Nimefika hapa na nimeridhishwa na kazi ya uendelevu wa mradi huu ambao umefikia asilimia 35,mradi huu wa kimkakati wa wizara, natoa maelekezo mahususi mkandarasi autekeleze kwa viwango vya ubora na thamani ya fedha na aongeze nguvu kazi ili ukamilike kwa wakati,wananchi wa Mwanza wapate maji na haitakuwa kuwa sawa wakati wako jirani na Ziwa Victoria halafu tuwaambie tuna changamoto ya maji,si sawa na hawatatuelewa,”alisema.

Waziri huyo wa maji alisema kutoka na umuhimu wa mradi huo, mkandarasi aongeze nguvu kazi ili kuhakikisha mradi wa Maji Butimba unakamalika kwa wakati, hivyo mkandarasi kampuni ya SOGER SATON iwalipe staki zao wafanyazi wanaofanya kazi kwa uaminifu wapate haki ya jaso lao. 

“Wananchi wa Jiji la Mwanza wana uhitaji mkubwa wa maji, tunataka mradi huu ukamilike wapate safi na salama,lazima muukalie kooni,ukikamilika utawapa heshima na kufanikiwa kwake ni mafanikio ya serikali,”alisema Awesso.

Alieleza kuwa,mahitaji ya maji Jiji la Mwanza ni lita milioni 160 kwa sasa zinazalishwa lita milioni 90 kupitia mitambo ya Capripoint ambapo kutokana na mahitaji makubwa na ongezeko la watu, wabunge wa Jiji hilo walipiga kelele kwa sababu ya maji.

Aidha alisema Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na uhusiano mzuri alipata fedha zaidi ya sh. bilioni 69 na kuzielekeza kujenga chanzo kipya cha maji Butimba ili kuongeza uzalishaji wa lita milioni 48 wananchi wa Nyamagana na Ilemela wapate huduma ya maji safi na salama ambapo wabunge  walimshukuru Rais Samia baada ya kutoa fedha hizo.

Kwa mujibu wa wa Awesso mradi huo umepangwa mkandarasi aukabidhi Februari mwakani wananchi wa Jiji la Mwanza wanufaike na kazi nzuri ya Rais wao,hivyo michakato isiyo ya lazima na variation katika mradi huo hatakubaliana nazo kwa sababu fedha zipo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele, alieleza kuwa mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita za maji milioni 48 kwa siku ambapo chanzo hicho kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 160 lakini wameanza na awamu ya kwanza ya mradi kabla kufanya upanuzi wa mradi kwa awamu tatu zilizobaki.

“Hatuna changamoto ya malipo na mkandarasi analipwa kwa wakati,mradi ulianza Februari 2021 na unajengwa kwa mfumo wa kusanifu na kujenga,tunategemea ukamilike Februari 2023, kwa sasa umefikia asilimia 35, lengo ni kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa maji kwa Jiji la Mwanza ili kuondoa changamoto ya upungufu uliopo wa huduma hiyo,”alisema.

Naye Mjumbe wa Bodi ya MWAUWASA Dkt.Elibariki Mmari,alimshukuru Rais Samia kwa kusikia kilio cha wananchi na kuleta mradi huo wa maji Butimba ingawa awamu tatu  zitajengwa baadaye,ukikamilika changamoto ya maji itabaki historia.

“Nikuombe mh. Waziri Awesso na wizara yako uone kwa namna gani utatafuta fedha za kukamilisha awamu zilizobaki za mradi huu ili kuondoa au kupunguza changamoto ya maji kwa sababu hapa tutapata lita milioni 48 ukijumlisha na zilizopo lita milioni 90 tutakuwa na lita milioni 138 hivyo upungufu bado utakuwepo,”alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post