WASHIRIKI WA MKUTANO WA WIPO USWISI WATEMBELEA UBALOZI



 Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa Geneva, Uswisi Mhe. Maimuna Kibenga Tarishi( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania ulipotembelea tarehe 22 Julai, 2022 katika ofisi za Ubalozi Geneva, Uswisi. Ujumbe huo ulioongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa(wa pili kutoka kulia), ulifika nchini humo kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 63 wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani, uliofanyika tarehe  17-21 Julai, 2022.  Wajumbe wengine  kutoka kushoto ni 

Mkuu wa Idara ya Uraghbishi kutoka Tume ya Ushindani (FCC) Bi. Magdalena Utouh, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali (BPRA) Zanzibar, Bi. Mariam Mliwa Jecha na Msajili Msaidizi Mkuu wa BRELA  Bi. Loy Mhando.

Post a Comment

Previous Post Next Post