WAZIRI BALOZI DKT CHANA AFANYA ZIARA YA KIKAZI SERENGETI.




                                  ………………

Na Sixmund Begashe wa MNRT

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amefanya ziara ya kikazi kwenye Hifadhi ya Taifa Serengeti Mugumu kwa lengo la kuhamasisha utalii na mwendelezo wa programu ya Royal Tour pamoja na kukagua maendeleo ya maandalizi ya ujenzi wa uwanja wa ndege Burunga.

Uwanja huo unaotarajiwa kujengwa katika eneo la hifadhi ya Serengeti utakapo kamilika utakuwa kichocheo kikubwa cha Utalii kwa kupokea watalii wengi na kuifanya Wizara ifikie lengo la Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufikisha idadi ya watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2020/2025.

Post a Comment

Previous Post Next Post