WAZIRI AWESO AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA EXIM BENKI YA INDIA



 *New Delhi, India*

Waziri wa Maji  Mhe. Jumaa Aweso (Mb)  amekutana na kuzungumza na Ms. Harsha Bangari, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya  India

Kikao hicho kimefanyika New Delhi,  India ambapo Mh. Aweso kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameishukuru Benki ya Exim ya  India kwa kushirikiana na Tanzania hususani katika Sekta ya Maji kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ikiwemo mradi mkubwa wa maji wa Tabora-Igunga-Nzega na Tinde-Shelui.

Aidha, amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya   Exim ya India kwa kuendelea na ushirikiano  katika utekelezaji mradi wa maji wa  kihistoria wa Miji 28 ambapo Benki hiyo imetoa zaidi ya  Dola za Kimarekani milioni 500. 

Katika hatua Nyingine, Waziri Aweso ameiomba benki hiyo kuendelea kushirikiana na kuiunga mkono kwa rasilimali fedha Tanzania  katika  kutekeleza miradi ya maji ya kimkakati na kutoa wasilisho lenye mapendekezo ya maeneo muhimu kwa sasa  na kusisitiza kwa pamoja kuendelea kudumisha mashirikiano baina ya Tanzania na India katika sekta muhimu ya Maji.

Katika hatua nyingine kwenye kikao hicho Mhe. Aweso amewasilisha    umuhimu na maono ya dhati ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwezesha upatikanaji wa Fedha kwa Tanzania katika katika kufanikisha jiji la Dodoma  kufanikisha mradi wa maji kutoa  Ziwa Victoria  kutokana na ongezeko la watu na  mradi wa Rufiji - Dar es salaam  ikiwa ni  hatua  ya kumaliza changamoto ya huduma ya maji katika majiji hayo.

Post a Comment

Previous Post Next Post