WAZIRI MCHENGERWA ATEMA CHECHE BBC


 Na John Mapepele, London

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania imefanya mapinduzi makubwa kwenye Michezo katika kipindi kifupi chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo Julai 29, 2022 kwenye mahojiano maalum na Idhaa ya kiswahili ya BBC katika studio zilizopo jijini London wakati akihojiwa na mtangazaji Zawadi Machibya.

Mhe. Mchengerwa amesema katika kipindi kifupi Tanzania imefanikiwa kuingiza timu nne kwenye mashindano ya dunia.

Aidha, amesema Tanzania inafanya uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ambapo inatarajia kuandaa mashindano makubwa ya michezo.

Kuhusu mkakati wa kuibua vipaji Mhe. Mchengerwa amesema tayari imeandaa program ya mtaa kwa mtaa.

Mhe. Mchengerwa amesema Serikali imefufua mashindano ya michezo kwa shule za msingi na Sekondari ili kuibua vipaji.

Ameongeza kuwa Serikali inakwenda kuchenga shule maalum za michezo na akademi za michezo.

Post a Comment

Previous Post Next Post