Dk.Ngailo:Kuna Fursa Katika Uwekezaji Mbolea Nchini

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dk.Stephan Ngailo akimuhudumia mwanachi wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Kilimo katika maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika Viwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dk.Stephan Ngailo akizungumza na waandishi wa habari  wakati alipotembelea Banda la TFRA  na kuzungumza kuhusiana huduma wanazozitoa katika  Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika Viwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Dkt. Stephan Ngailo akisikiliza maelezo kutoka kwa  Meneja wa Kitengo cha Uhusiano, Mawasiliano na Elimu kwa Umma Matilda Kasanga wakati Mkurugenzi Mtendaji huyo  alipotembelea Banda la TFRA   katika  Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika Viwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Mahitaji ya Mbolea ni makumbwa  nchini hivyo Wawekezaji wa ndani na nje wana fursa katika sekta ya mbolea  na uwekezaji huo unalipa  wa kufanya fedha zao zirudi bila  changamoto yeyote.

Akizungumza Julai 8,2022 katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu SabaSaba yanayaofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Mkurugenzi Mtendaji  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania ( TFRA),Dk. Stephan Ngailo  amesema soko la mbolea ni kubwa hapa nchini na hata nchi zinazoizunguka Tanzania ambapo  viwanda vikiwekezwa vinaweza kuhudumia nchi zinazotuzunguka.

Dk.Ngailo amesema kuwa sekta ya mbolea ina utashi wa kisiasa uliopo kwani mahitaji ya mbolea ni makubwa na Rais kafungua mipaka ya mahusiano ya kidiplomasia ya kuvutia uwekezaji nchini.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa Tanzania ni kitovu cha mbolea katika nchi wanachama wa Jumuiya ya ya Nchi za Afrika zilizo Kusini  mwa Jangwa la Sahara (SADC) ambapo Soko la mbolea lina fursa kubwa kutokana nchi hizo kwa asimilia kubwa inategemea kilimo.

"Watu wanaongezeka na Ardhi inabaki pale pale lazima tuongeze tija kwa kuzingatia kanuni bora za  matumizi sahihi ya mbolea katika kuongeza mapato ya mavuno" amesema.

Akizungumzia maonesho ya Sabasaba amesema  Dk. Ngailo ameeleza kuwa lengo la kushiriki maonesho ni kuchukua TFRA na kuipeleka kwa Umma waweze kutoa elimu  pamoja na majukumu ya  tasnia ya mbolea zote zinazozalishwa hapa nchini na kuhakikisha zina aksi  ubora na viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Awali Kaimu Meneja Huduma za Sheria kutoka TFRA Belinda Kesi amesema wamekuwa wakihamasisha wao kuzingatia matakwa ya kisheria yaliyowekwa watu wasipozingatia viwango vya mbolea wanaigharimu nchi.

"Kama mdau anataka kuingia katika tasnia ya mbolea ahakikishe anatambulika na Mamlaka husika kisheria, jukumu letu ni kusimamia tasnia hii pamoja na majukumu mengine," amesema

Ameongeza kuwa TFRA imeanzishwa mwaka chini ya Sheria Namba 9 ya mwaka 2009 ikiwa na jukumu la kusimamia tasnia ya mbolea nchini pamoja na majukumu mengine ni kuhakikisha mbolea hiyo inayotumika, inayoingia, inayosafirishwa nje ya nchi inakuwa katika ubora unaotakiwa na vigezo vya biashara vinazingayiwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post