MILANGO IPO WAZI UWEKEZAJI KWENYE SEKTA MISITU.



 ……………………..

NA Sixmund Begashe NMRT

Wadau wa ndani na nje ya nchi wamehamasishwa kuwekeza kwenye Sekta ya Misitu kwa kuwa sekta hiyo inakuwa kwa kasi kutokana na mahitaji yake kuwa makubwa kwa jamii.

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana ametoa hamasa hiyo wilayani Mufindi alipotembelea kiwanda cha kutibu Mazao ya Misitu cha Green Resources Sao Hill ambapo amesisitiza kuwa milango ipo wazi kwa yeyote aliye tayari.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira mazuri na salama kwa wawekezaji hivyo ni wakati wa wadau kuchangamkia fursa mbalimbali zilizo katika sekta ya Misitu.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Kiwanda hicho Bw. John Rabie ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuiimarisha Sekta ya Misitu hali inayochangia upatikanaji wa malighafi ya kiwanda hicho kwa uhakika na haraka.

Akiwa katika kiwanda hicho cha Sao Hill, Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana ameshuhudia namna mazao ya misitu yanavyokaushwa na kuwekewa dawa kwa ubora.

Mhe. Balozi Dkt. Chana ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kazi nzuri akiahidi Wizara anayoiongoza itaendelea kutoa ushirikiano unahitajika.

Post a Comment

Previous Post Next Post