Na John Mapepele
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Maji na Madini nchini Burundi ndugu Selemani Khamissi ambaye pia ni mmiliki wa kikundi maarufu cha taarabu nchini humo cha Alwatan kinachoshiriki kwenye Tamasha la Kitaifa la Utamaduni ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuandaa tamasha hilo huku akisisitiza kuwa tamasha hilo litaitangaza vema Tanzania duniani.
Akiongea na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na michezo. Saidi Yakubu ofisini kwake jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili amesema Serikali ya Burundi inaunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania katika kuenzi na kuendeleza utamaduni ndiyo maana wasanii kutoka Burundi wanashiriki katika tamasha hili.
“Naomba nisema nimefurahi kuja Tanzania kushiriki kwenye tamasha tunawahidi watanzania wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuja kuona uzoefu wetu kwenye taarabu kwa kuwa Burundi ina hazina kubwa ya magwiji wa taarabu kutoka miaka mingi.”amesisitiza Khamissi
Akiwa ofisini hapo Khamissi amepata fursa ya kutembelea Uwanja wa Benjamin Mkapa pia kuangalia maandalizi yanayoendelea ambapo ameelezea kuwa uwanja huo una hadhi ya kimataifa.
Akimtembeza kwenye miundombinu ya uwanja hui Yakubu amesema maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo yamekamilika