Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetakiwa kutoa Elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kulinda maeneo yaliyohifadhiwa ili waache tabia ya kuyavamia na kuanzisha makazi na shughuli nyingine za kibinadamu kama Kilimo na ufugaji.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana (Mb) alipokutana na Naibu Kamishna anaesimamia Kanda ya Mashariki, Steria Ndaga, ofisini kwake.
Mhe. Chana amesema si vyema kuona migogoro kati ya wanyama na watu walio vamia maeneo ya Hifadhi inaendelea, hivyo ipo haja ya haraka ya kuielimisha jamii juu ya ukweli kuhusu namna bora ya kuepukana na migogoro hiyo hasa kwa wanaofanya kazi za kijamii kwenye mapito ya wanyamapori.
Licha ya kuzungumzia fursa zitakazo tokana na Filamu ya Royal Tour, Mhe. Chana ameutaka uongozi wa Shirika hilo kuhakikisha unakaa na wananchi majirani na Hifadhi pamoja na wadau mbalimbali kuwaelimusha juu ya namna ya kuchangamkia fursa hiyo kwa kueekeza katika huduma za Malazi, vyakula, na mazao mengine ya Utamaduni.
Akizungumza kuhusu changamoto wanazokutana nazo Naibu Kamishna anaesimamia Kanda ya Mashariki, Steria Ndaga amesema kuwa ni pamoja na Utalii wa bure unaofanywa na wenye magari yanayopita Hifadhini na kuisababishia Serikali kupoteza mapato makubwa, Moto na ukame.
Akiwa katka Hifadhi ya Mikumi Mhe. Chana amepata nafasi ya kutembelea vivutio vya Hifadhi hiyo na kujionea utajitri Mkubwa wa wanyamapori, mimea mbalimbali pamoja na ukarabati unaoendelea wa uwanja wa ndege