TFRA YASHEHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA KUWAKUMBUSHA KUFANYA KAZI KWA UELEDI NA BIDII


Kaimu Meneja Uhusiano mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania  (TFRA )Matilda Kasanga akieleza namna wanavyosheherekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

ya Pamoja ya wafanyakazi wa kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania  (TFRA ) wakisheherekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani

…………………………………

NA MUSSA KHALID

Wanawake nchini wamekumbushwa kendelea kufanya kazi kwa ueledi,bidii pamoja na uadilifu ili kujipatia kipato na  kuongeza tija katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Meneja Uhusiano mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania  (TFRA ) Matilda Kasanga wakati akifanya mahojiano na mwandishi nwa habari hizi ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.

Akianza kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan,Matilda amesema amekuwa mfano wa kuongeza imani kwa wanawake wa Tanzania kutokana na kuwa kiongozi katika nafasi ya Juu ya nchi.

Matilda amesema kuwa katika nafasi ya familia mwanamke ndiye mlezi mkubwa kwa kujenga maadili na malezi kwa watoto akishirikiana na baba hali ambayo inamfanya andelee na mchango mkubwa katika jamii.

‘Mwanamke amekuwa mlezi kwani wote tumetokana na mama tangu tumboni mpaka tunazalisha walimu,viongozi na madaktari hivyo hiyo nafasi tu inamfanya mwanamke aheshimike kwenye jamii na aonekane ni mtu mwenye mchango mkubwa sana kwenye jamii’amesema Matilda

Aidha amewataka wanawake kuwa katika kuadhimisha siku hiyo,ni vyema wakajikita katika ufanyaji wa kazi mbalimbali kwani wananafasi kuwa katika kuleta chachu kubwa katika maendeleo ya nchi.

‘Niendelee tu kumshukuru Mhe Rais kwa kututia ujasiri kwa sababu ameonyesha njia kuwa Mwanamke anaweza ukiangalia katika Afrika Mashariki na Afrika ni miongoni mwa marais wa chache Duniani kwa hiyo nafasi yake pale alipo anapotuonyesha njia na sisi ndivyo tunavyopata ujasiri’amesema Matilda

Katika Hatua nyingine Kaimu Meneja Uhusiano Huyo wa TFRA amewahimiza wakulima na watanzania kutumia mbolea ili kuongeza tija katika uzalishaji katika sekta hiyo

 

Post a Comment

Previous Post Next Post