WAZIRI JAFO AANIKA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

  

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo March 2,2022 jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita madarakani.

Viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita madarakani,leo March 2,222 jijini Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akionesha kitabu cha Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 kwa zungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita madarakani,leo March 2,2022  jijini Dodoma

…………………………………..

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza leo March 2,2022 jijini  na waandishi wa habari alisema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja cha Serikali Ofisi ya Makamu wa Rais imeboresha mfumo na taratibu za utoaji wa vibali vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa kutoa miongozo ya namna ya kutekekleza agizo la utoaji wa vibali husika ndani ya siku 14 baada ya kupokea Taarifa ya mwisho kutoka kwa Mwekezaji. 

Dkt. Jafo alisema kuwa katika kipindi hicho, jumla ya vibali 1445 vimetolewa ikiwemo vibali 1014 vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na vibali 431 vya Ukaguzi wa Mazingira.

Aliongeza kuwa katika Miradi Ya Hifadhi ya Mazingira, Ofisi imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya hifadhi ya mazingira ikiwemo, Mradi wa Kurejesha Ardhi Iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula Katika Maeneo kame ya Tanzania (Reversing Land Degradation and Food Security in Semi-Arid Areas – LDFS.

Post a Comment

Previous Post Next Post