MSD KUWA MKOMBOZI USAFISHAJI DAMU KWA WAGONJWA WA FIGO

Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi  akifungua mafunzo  ya waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya siku ya figo duniani , itakayofanyika  machi,10 mwaka huu kulia ni Mratibu wa Mgonjwa ya Figo, Wizara ya Afya, Dr Linda Ezekiel, mafunzo hayo yamefanyika kwenye ofisi za Bohari  Kuu ya Dawa Keko.
Mratibu wa Magonjwa ya Figo, Wizara ya Afya, Dr Linda Ezekiel akiwasilisha mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya figo duniani , itakayofanyika  machi,10 mwaka huu
Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa Meja Jen. Dkt. Gabriel Sauli Mhidize akitoa salamu zake kwa waandishi wa habari waliohudhuria katika mafunzo hayo.
Mdhibiti Ubora kutoka Bohari kuu ya Dawa(MSD) Joseph Kitukulu akiwasilisha mada kuhusu mashine zinazotmika kusafisha figo za wagonjwa
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bohari Kuu ya Dawa MSD Bi. Etty Kusiluka kulia akifafanua jambo mara baada ya Mratibu wa Mgonjwa ya Figo, Wizara ya Afya, Dr. Linda Ezekiel akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.
Picha mbalimbali zikiwaonesha waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo hayo yaliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Bohari  ya Dawa MSD Keko jijini Dar es Salaam.
                      ………………………………………

UAGIZWAJI wa mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji uliofanywa na Bohari Kuu ya Madawa(MSD) unaelezwa utapunguza kwa nusu ya gharama za kupata huduma hiyo hapa nchini.

Mratibu wa Mgonjwa ya Figo, Wizara ya Afya, Dr Linda Ezekiel amebainisha hayo kwenye mafunzo  kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya siku ya figo, machi,10 mwaka huu.

Amesema kuwa mara ufungaji wa mashine ukikamilika, husuma hiyo itapatikana katika hospital zote za serikali.

Dkt. Ezekiel alisema kuwa Serikali kupitia Bohari Kuu ya Madawa(MSD) imeagiza tayari mashine 171 za kusafisha damu,mashine za kuchakata maji 11,mashine za kuchakata vitenganishi vya unga 26.

” Katika kipindi cha mwaka mmoja cha awamu ya sita, serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilion moja katika huduma za usafishaji damu.Matarajio ni kuwa baada ya ufungaji wa mashine hizo huduma itapatikana kwa gharama nafuu zaidi,”alisema.

Ameaongeza kuwa ugonjwa wa figo ni tishio kwa sasa  kwani unahitaji rasilimali nyingi ili kupata huduma za afya.

Daktari huyo bingwa alisema takwimu zinaonyesha kuwa kuna takribani wagonjwa 1000 wana matatizo ya figo nchini.

amebainisha  kuwa kati ya wagonjwa  5800 and 8400 wanaohitaji huduma ya kusafisha damu, 2750 tu wanapata huduma hiyo.

Naye Mdhibiti Ubora kutoka Bohari kuu ya Dawa(MSD) Josepgh Kitukulu amesema kuwa serikali inatumia zaidi ya billion 29,484  kwa mwaka kufanya huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa 1000.

Katukulu amesema  kupitia Bohari Kuu ya Dawa itaokoa   zaidi ya bilioni 13.338 na hivyo kuboresha upatikanaji wa huduma nyingi zinazoambatana na hizo.

 “Mipango yetu ni kuona watu wanapata huduma hii ya usafishaji damu katika bei nafuu,” alisema Katukulu.

Kila ifikapo tarehe 3 mpaka 7 kila mwaka, Tanzania inaungana na nchi nyingine kuadhimisha siku ya figo duniani

Post a Comment

Previous Post Next Post