TAMASHA LA SERENGETI 2022 LAFUNIKA

Na. John Mapepele

Wakati tamasha la Serengeti linaingia siku ya pili, dhana ya   Tamasha hilo kutumia Sanaa  kuutangaza Utamaduni na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini leo umedhihirika wazi kwa kikundi cha kimasai kutoka Arusha kutoa burudani kali mbele ya  maelfu ya mashabiki.

Kundi hili lililochanganya wanawake na wanaume wamelivamia jukwaa  wakiwa kwenye mavazi maalum ya kimasai na kufanikiwa kuuchezesha umati huo.

Pamoja na kuvalia kimasai kundi hili liliweza kutumbuiza nyimbo za mitindo mbalimbali kutokana na mahitaji ya wapenzi.

Wasanii zaidi ya hamsini wanatarajiwa kupanda ikiwa ni pamoja na Harmonize ambapo hadi sasa  baadhi ya wasanii waliopanda ni pamoja na Stara Thomas, Mzee Yusuf na Mrisho Mpoto ambaye alighani mistari ya kuisifia Tanzania






Post a Comment

Previous Post Next Post