STAMICO WAUNGANA NA WANAWAKE DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

 


Watumishi wanawake wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika maandamano walipoungana na wanawake wengine  duniani kote kuadhimisha siku ya wanawake duniani katika viwanja vya Uhuru jiji Dar es Salaam ambapo maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Visiwani Zanzibar ikiwa mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani maadhimisho hayo yamefanyika leo duniani kote
Mmoja ya wafanyakazi wanawake walipotembelea kiwanda chakutengenezea mkaa wa mawe kilichopo msasani jijini Dar es Salaam Latifa Abdallah akiuliza swali kwa Mhandisi Happy Mbenyange wakati walipotembelea kiwanda hicho wakiadhimisha siku ya wanawake Duniani yaliyohitimishwa leo,
Mhandisi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)  Happy  Mbenyange   (kushoto), akitoa maelekezo kwa baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Shirika la hilo walipotembelea kiwanda chakutengenezea mkaa wa mawe rafiki kwa mazingira kilichopo msasani jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyohitimishwa leo duniani kote
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO  wakiwa katika picha ya pamoja
************************
Na Stella  Kessy
KATIKA Maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani   Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya Sita kwa jitihada za kuwawezesha Wanawake katika sekta mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mhandisi wa(STAMICO) Pili Athumani  amesema katika shirika la madini limezingatia hilo kwa kuwapa kipaumbele  mwanawake  na kutoa majukumu sawa na wanaume ili kutekeleza kauli mbiu ya Siku ya wanawake.
“Kampuni yetu inathamini sana wanawake,kwani kwa kulingana na kauli mbiu ya mwaka huu ni  ‘kizazi cha haki na usawa  kwa maendeleo endelevu kwa jamii’ katika sekta ya madini suala hili limepewa kipaumbele, kwani wanawake wamekuwa wanapewa kipaumbele katika kusimamia miradi”Amesema.
Ameongeza kuwa katika sekta ya madini mwitiko wa wanawake umekuwa mwingi  katika shughuli zote za madini Wanawake wengi wamekuwa wakijitokeza na kujiari na wanazitumikia fursa kama ifuatavyo.
“katika shirika letu la madini sisi Kama wanawake waandisi tumekuwa tukipewa majukumu kama wanaume kwahiyo wanaitekeleza hiyo kauli mbiu  ipasavyo kwani tunaopewa miradi mingi ambayo tunasimami na kutendea haki kadri ya uwezo wetu na kuifanikisha na kutoa matokeo chanya”
Pia ametoa wito kwa serika endelee kutuamini sisi wanawake kwa kupewa majukumu mbalimbali kwani wanawake tunaweza.

Post a Comment

Previous Post Next Post