Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) Bi, Latifa Mohamed Khamis pamoja na Mrajisi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dr.Benson Ndiege leo tarehe 23 Machi, 2022 katika Ofisi za Tume jijini Dodoma wamesaini makubaliano yenye lengo la kuwawezesha wana ushirika na wakulima kupitia Vyama vya Ushirika nchini kuzalisha bidhaa zao kwa tija ili kufikia masoko endelevu .
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi.Latifa amebainisha kuwa Progamu hiyo inalenga kuongeza thamani za bidhaa za ndani na kisha kuwaendeleza wazalishaji na hatimaye waweze kuwa na uwezo wa kutumia fursa za biashara na masoko ya ndani na nje ya nchi
Pande zote mbili Kwa pamoja zimeridhia kuwa na mabadiliko ya kasi katika sekta ya biashara ili kwenda sambamba na Serikali ya awamu ya Sita inayohimiza uongezwaji wa thamani kwa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini ili kuwaletea wananchi maendeleo yenye tija.
Kwa Upande wake Dr.Benson Ndiege Wamevisihi Vyama vya Ushirika nchini kuhakikisha vinashiriki kikamilifu katika programu zilizoainishwa katika makubaliano haya kwa kuunga mkono jitihada za Mhe. rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuleta mabadiliko kwenye uchumi wa nchi yetu kuwafikia walengwa .
Makubaliano hayo yanalenga ushirikishwaji katika programu za TanTrade za kukakikisha bidhaa za Vyama vya Ushirika zinapatiwa masoko endelevu ambapo wanachama wa vyama vya ushirika watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo Pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa zao.