Na Mwandishi wetu-MOI
Waziri wa Afya Mh.Ummy Mwalimu (MB) leo 21/03/2022 amezindua kongamano la 8 la kimataifa la mafunzo ya madaktari bingwa wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu.
Kongamano hilo limeratibiwa na MOI kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Weill Cornel cha Marekani.
Mh.Ummy amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika Taasisi ya MOI jambo ambalo limepelekea kuimarika kwa utoaji wa huduma za kibingwa kwa wananchi.
‘’Hospitali yetu ya MOI kwa sasa ina vifaa vya kisasa vya MRI, CT-Scan na maabara ya kisasa ya upasuaji na ubongo haya ni baadhi ya mageuzi makubwa ambayo yamefanywa hapa na Serikali Alisema Mh Ummy
Aidha, Mh. Ummy amesema Serikali ya awamu ya sita itaendelea kutoa ufadhili kwa madaktari bingwa wa ubongo , mgongo na mishipa ya fahamu wakapate mafunzo ndani na nje ya nchi ili kukabiliana na uhaba na wataalam hao hapa nchini.
Kwa Upande wake Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt Respecious Boniface amesema hili ni kongamano la 8 ambapo zaidi ya madaktari 150 pamoja na wauguzi 100 kutoka katika mataifa mbalimbali wanashiriki.
‘’Kongamano hili lintafanyika katika mfumo wa nadharia na vitendo, hivyo tunatarajia zaidi ya wagonjwa 25 watafanyiwa upasuaji wa ubongo, mgongo kwa mbinu za kisasa” Alisema Dkt Boniface.
Dkt Boniface amesema pamoja na mambo mengine washiriki watafundishwa mbinu mpya za upasuaji wa ubongo , mongo na mishipa ya fahamu kwa njia ya kisasa ili waweze kuwapatia wagonjwa huduma za kisasa.
Kongamano hili ni sehemu ya mkakati wa Taasisi ya MOI wa kuhakikisha wataalamu hapa nchini wanapata huduma bora za kibingwa za Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu.
Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu (MB) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano la kimataifa la mafunzo ya madaktari bingwa wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu, kongamano linafanyika kwa siku tano katika taasisi ya MOI.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu.
Washiriki wa Kongamano la 8 la madaktari wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya fahamu wakifuatili mada leo katika ukumbi wa mikutano MOI, Kongamano hilo limezinduliwa na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu (MB).
Mkufunzi kutoka Chuo kikuu cha Marekani Prof. Roger Hartl akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu,