Mhe.Mchengerwa: Tanzania na China ni marafiki wa kihistoria

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa  amesema Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na wa muda mrefu   ulioasisiwa na viongozi wa mataifa hayo mawili ambao hauna budi  kuendelezwa na kurithishwa vizazi hadi vizazi. 

Mhe.Mchengerwa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam aliposhiriki pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe.Chen Mingjian kwenye hafla ya Uzinduzi wa Mashindano ya Olympic ya michezo ya majira ya baridi yanayozinduliwa rasmi leo Februari 4, 2022 jijini Beijing kwa kucheza mchezo wa  mpira wa meza kwenye Ubalozi wa China nchini Tanzania.

"Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na wa muda mrefu kwenye Sekta  za Utamaduni, Sanaa na Michezo ulioasisiwa na viongozi waanzilishi wa mataifa hayo mawili ambao umekua na manufaa ikiwemo upatikanaji wa fursa za kutangaza utamaduni na lugha za mataifa haya kwa nchi hizi mbili" amesema Mhe.Mchengerwa.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,   Mhe. Samia Suluhu Hassan ana matarajio makubwa ya mahusiano wa nchi hizi mbili katika sekta za wizara yake.

Katika hafla hiyo Mhe. Balozi na Mhe. Waziri wamekubaliana   Wizara kuandaa andiko la mashirikiano ( MoU) katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuziendeleza sekta hizo.




Post a Comment

Previous Post Next Post