YADHIBITI UBORA WA MBOLEA ZINAZOINGIA NCHINI

 

**********

·          Tani 259,170  zakaguliwa

 

Imeelezwa kuwa, Jumla ya
tani 259,170 za mbolea zilizoingizwa kutoka nje ya nchi zilikaguliwa na 
kuhakikisha kuwa mbolea wanayouziwa
mkulima inakidhi viwango vya ubora
 ili kuleta tija katika shughuli za kilimo nchini.

 

Ukaguzi huo uliofanyika
katikaia kipindi cha Julai hadi Disemba 2021 ni moja kati ya majukumu makubwa yanayofanywa
na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) ya kuhakikisha  kuwa  
biashara ya mbolea nchini
inakidhi matakwa ya viwango bya ubora wa
mbolea.

 

Hayo yamebainishwa na
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti Gerod Nganilevanu alipokuwa akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji kwa Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya taasisi hiyo
katika kikao kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.  

 

Aidha, Nganilevanu alibainisha kuwa katika
kipindi cha Julai 2021 – Disemba 2021, Mamlaka imefanya ukaguzi katika mikoa 26
ambapo jumla ya wafanyabiashara 2,031 sawa na asilimia 129 ya lengo
wamekaguliwa.

 

Ameeleza kuwa, katika
kipindi cha Julai 2021 – Disemba 2021 jumla ya wafanyabiashara 2,031
walikaguliwa. Kati ya wafanyabiashara hao, 1,151 (57%) walikuwa na leseni hai,
194 (10%) walikuwa na leseni zilizoisha muda wake na 686 (33%) hawakuwa na
leseni kabisa, hivyo Mamlaka ilihakikiisha wafanyabiashara hao  wanapatiwa elimu na kasha kupewa leseni. 

 

Aliendelea kueleza kuwa,
kufuatia ukaguzi huo mamlaka ilibaini kuwa jumla ya wafanyabiashara 880 sawa na
asilimia 43 ya wafanyabiashara wote waliokaguliwa kwa kipindi cha hicho  walijihusisha na biashara ya mbolea bila kuwa
na leseni.

 

Akielezea hatua
zilizochukuliwa, Nganilevanu alisema mamlaka imewasaidia wafanyabiashara wote
waliokuwa na viambatisho stahili kuingia kwenye Mfumo wa Kimtandao wa Mbolea
(FIS), ambapo takribani wafanyabiashara 343 waliokuwa hawana leseni kwa kipindi
cha robo ya kwanza na ya pili waliweza kupata leseni za usajili.

 

Pamoja na hayo,
Nganilevanu alieleza kuwa katika kipindi cha Julai – Disemba 2021 wakaguzi wa
mbolea walipokuwa wakifanya ukaguzi  katika mikoa ya Arusha, Kigoma na Tabora walibaini
uwepo wa mbolea tisa (9) za kimiminika
sokoni ambazo hazikusajiliwa na mamlaka hiyo.

 

Alizitaja  Mbolea hizo kuwa  ni  Mawenzi Ansil booster, New power Booster,
Top max crop leader, Vita booster, Tanzanite, Max golden Bloomv Plus N,
Mokusaku brix, Herbolive,
 Suber AGROFOLIAR
(NPK 23:23:23+TE)

 

Kufuatia hali hiyo
mamlaka iliziondoa sokoni Mbolea hizo wafanyabiashara kupewa amri ya kuacha
kuuza (stop sale order) mbolea hizo.

 

Akihitimisha wasilisho
lake, Nganilevanu alisema pamoja na hatua zilizochukuliwa kwa wafanyabiashara
wanaokiuka matakwa ya kisheria ya utengenezaji na biashara ya mbolea, mamlaka
imeandaa Mpangokazi kwa ajili ya kufuatilia wafanyabiashara wote waliobainika
kufanya biashara kinyume na taratibu za sheria ya mbolea.

Hata hivyo, Mpangokazi
huo umezingatia katika kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wote ambao hawana
mafunzo na vyeti vya mafunzo ili waweze kukidhi kigezo cha kufanyiwa usajili.

Post a Comment

Previous Post Next Post