VIJANA WA SONGWE WAISHUKURU SERIKALI RUZUKU YA MBOLEA


 Mwandishi Wetu,

Mkulima kijana kutoka Kijiji cha Chiwezi, Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe, Bw. Nestory Kawia, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa katika kuboresha sekta ya kilimo kupitia mpango wa ruzuku ya mbolea.

“Tunamshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya. Ameweza kutuwekea ruzuku ya mbolea, na sasa bei ni nafuu, inatufaa sisi wakulima. Inatusaidia kupata kipato chenye tija na mavuno kuwa mengi,” amesema Bw. Kawia.

Ameeleza kuwa kupatikana kwa mbolea kwa bei nafuu kumeongeza uwezo wa wakulima wengi kulima kwa tija, hali iliyoongeza uzalishaji wa mazao na kipato cha kaya vijijini.

Bw. Kawia ametoa wito kwa vijana wenzake nchini kuachana na dhana kwamba kilimo ni kazi ngumu, akisisitiza kuwa kilimo cha kisasa chenye kutumia pembejeo bora kinaweza kubadilisha maisha yao.

“Nawashauri vijana wenzangu tujikite kwenye kilimo; kilimo kinalipa, kinakutoa sehemu moja kwenda nyingine,” ameongeza.



Post a Comment

Previous Post Next Post