Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewasilisha ombi la kusaidiwa ujenzi wa Viwanja kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian.
Mhe. Mchengerwa ametoa ombi hilo alipokutana na Balozi huyo leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Uzinduzi wa Mashindano ya Olympic ya michezo ya majira ya baridi yanayozinduliwa rasmi leo Februari 4, 2022 jijini Beijing.
"Nitumie nafasi hii kukuomba Mhe. Balozi Chen kama ambavyo China imekua msaada katika mambo mbalimbali kwa nchi yetu, nakusihi utusaidie katika mkakati wa Serikali yetu wa kuimarisha miundombinu ya michezo hususan viwanja vya michezo ili Tanzania pia ipige hatua kwenye michezo"amesema Mhe. Mchengerwa.
Aidha, Mhe.waziri ameiagiza Kamati ya Olympic nchini kujipanga na kuandaa wachezaji ambao mwakani watakwenda kushindana, siyo kutalii.
Amepongeza Nchi ya China kwa kuanza mwaka mpya na kumpongeza Balozi huyo kuteuliwa kuiwakilisha nchi yake hapa Tanzania.