Mhe. Mchengerwa aiomba China kusaidia kutangaza Kiswahili

 

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameiomba nchi ya China kusaidia kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili duniani kutokana na Taifa hilo kuwa na ushawishi mkubwa.

Mhe. Mchengerwa amewasilisha ombi hilo baada ya kukutana na Balozi wa China nchini Tanzania. Mhe, Chen Mingjian katika hafla ya Uzinduzi wa Mashindano ya Olympic ya michezo ya majira ya baridi yanayozinduliwa rasmi leo Februari 4, 2022 jijini Beijing.

"Ni mategemeo yetu kuwa mtawachukua wataalam  wetu wa kiswahili ili wakafundishe katika vyuo vyenu vikuu" amesisitiza  Mhe. Mchengerwa.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Chen  amesema,  nchi yake inaitazama Tanzania kama rafiki wa kwanza katika Bara la Afrika na kwamba imekuwa na mabadilishano ya watu kuja kujifunza na mafunzo mbalimbali kabla ya corona. 



Post a Comment

Previous Post Next Post