Mhe. Mchengerwa apongeza ubunifu wa wadau wa tamasha la Sauti za Busara

Na. John Mapepele 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewapongeza  wadau mbalimbali wa Sanaa walioshiriki kwenye tamasha la Sauti za Busara Zanzibar kwa ubunifu wao na  kuwataka waendelee kutumia  matamasha hayo kutangaza  bidhaa na huduma wanazozitoa.

Mhe. Mchengerwa  ametoa wito huo alipotembelea   mabanda yaliyokuwa yakionesha bidhaa na huduma zao kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Februari 13, 2022.

Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Mhe. Simai Mohamed Said ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kutembelea wadau wa  tamasha hilo huku akisisitiza kuwa  kitendo hicho kimeonesha anathamini mchango wa wadau hao.

Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotion, Sinai Mohamed Said  akimtambulisha Mhe. Mchengerwa kwa mmoja wa wadau kwenye banda la Benki ya CRDB
Mhe. Mchengerwa akiwa na kikosi cha mfalme wa Singeli nchini Sholo Mwamba kabla ya kikosi kupanda jukwaani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotion, Sinai Mohamed Said  akimpatia zawadi ya fulana Mhe. Mchengerwa wakati alipotembelea kwenye banda la  wandaaji

Mhe. Mchengerwa akiangalia kwa makini namna ambavyo  kikosi cha Ma DJ  kinavyofanya kazi ya kuburudisha umati iliofika kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara, Zanzibar

Post a Comment

Previous Post Next Post