Mhe. Mchengerwa aikaribisha dunia Tamasha la Serengeti kupitia Sauti za Busara

 Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewakaribisha  wageni mbalimbali waliohudhuria tamasha  kubwa  la kimataifa la Sauti za Busara  kutoka  sehemu  mbalimbali duniani kushiriki kwenye  tamasha la kihistoria  la muziki la Serengeti litakali fikia kilele chake Machi 12, mwaka  huu jijini Dodoma.

Akizungumza kwenye kilele  cha Tamasha la Sauti za Busara usiku wa kuamkia leo  Februari 14, 2022 huko zanzibar amesema  Serikali inakwenda  kuandaa matamasha makubwa  ya kihistoria ambayo yataonesha  utamaduni wa  kitanzania, hivyo dunia inakaribishwa kushuhudia tukio hili la kihistoria na kimataifa.

"Naomba kutumia nafasi hii  kuwakaribisha  kwenye  Tamasha la Serengeti na Tamasha la kimataifa la Sanaa na Utamaduni  la Bagamoyo ambayo yanakwenda  kuionyesha dunia  utajiri wa utamaduni  na vivutio vya utalii duniani". Ameongeza Mhe. Mchengerwa.

Mhe. Mchengerwa pia aliambatana na Katibu Mkuu wake,  Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi wa Sanaa . Dkt. Emmanuel Ishengoma.

Amepongeza Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo kwa  kuandaa Tamasha hilo kwa  kiwango cha kimataifa na kusisitiza  kuwa Serikali itashirikiana nao ili kuhakikisha tamasha lijalo linafanyika.

Mhe. Mchengerwa akiongea na umati wa wageni walioshiriki kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara Februari 13, 2022 Zanzibar
Mhe. Mchengerwa akitambulishwa na kamati ya maandali ya tamasha la Sauti za Busara ili aongee na umati wa watu walioshiriki kwenye kilele cha tamasha hilo usiku wa kuamkia leo Februari 14, 2022 Zanzibar
Wasanii mbalimbali wakitumbuiza kwenye kilele cha tamasha la Sauti za Busara huko Zanzibar, Februari 13, 2022

Waziri Mchengerwa akiteta jambo na Katibu Mkuu wake Dkt.Hassan Abbasi mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha  Tamasha la Sauti za Busara, huko Zanzibar Februari 13, 2022.





Post a Comment

Previous Post Next Post