MCHENGERWA ASHINDA NAFASI YA MNEC MKOANI PWANI, ASEMA ANA DENI LA KULIPA

 Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

Mohammed Mchengerwa ameibuka kidedea nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia mkoa wa Pwani,(MNEC) kwa kuchaguliwa kwa kura 792 ikiwa ni sawa na asilimia 92.

Akishukuru kupata nafasi hiyo ,amewaahidi wanachama kushirikiana kuimarisha na kuongeza uhai wa Chama.

Mchengerwa alieleza, hana cha kuwalipa wajumbe wa mkutano mkuu na wanachama ila amewiwa na deni la kuwalipa.

"Kura 792 nilizopata ni sawa na asilimia 92 inaonyesha namna mlivyokuwa na Imani na mimi ya kuwatumikia, sisi kama chama ,na dhamira ninayoifikiri ,Mwenyekiti na wajumbe tuliochaguliwa leo ni kwenda kukiimarisha chama na kuongeza uhai wa Chama"alielezea Mchengerwa.

"Yote hayawezekani ila ni kufanya kazi kwa bidii, kwa kufikika kuanzia tawi, mashina, kata,wilaya ,lazima tuwe na Chama imara na kuongeza idadi ya wanachama ,na kuongeza Imani kwa kuingia katika mioyo ya wananchi kuwatumikia na kuwa kioo kuwaletea maendeleo.

Awali msimamizi wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Pwani, Zainab Telaki alieleza,aliyeshinda MNEC ni Mchengerwa aliyepata kura 792 dhidi ya wagombea wengine Mbaraka Kitwana Dau, Muhammed Mussa Mtuliakwaku, Alhudi Shilla na Nunu Daudi Kanza.

Pia alitaja ,nafasi ya mjumbe Halmashauri Kuu CCM mkoa wa Pwani kutokea Kibaha Mjini alishinda Catherine Katele na Mussa Mansoor Said.

Kwa upande wake Mansoor aliwashukuru wajumbe na kueleza anahitaji ushirikiano, umoja na ushirikishwaji ndani ya Chama.

Post a Comment

Previous Post Next Post