WATUMISHI TFRA WATOA MSAADA KWA WAZEE WASIOJIWEZA





  Afisa udhibiti Ubora  kutoka TFRA Wambura Sostenes akiwa katika uso wa furaha na mmoja wa wazee wa Makazi ya Funga Funga Mkoani Morogoro mara baada ya TFRA kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali.

……………..

Katika jitihada za kurudidha fadhila kwa jamii wstumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa wazee wasiojiweza wanaoishi katika makazi ya Funga Funga yaliyoko katika Manispaa ya Morogoro Mjini.

Watumishi hao waliungana na washiriki wa mafunzo ya wakaguzi wa mbolea yaliyofanyika kuanzia tarehe 14 hadi 18 Novemba 2022 mkoani Morogoro, ambapo walikubaliana kwa pamoja kuchanga fedha kwa kadri walivyojaliwa ili kununua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia wazee hao.

Mahitaji yaliyokabidhiwa kwa wazee hao wa makazi ya Funga Funga ni pamoja na Mchele kilo 50, mafuta ya kupikia lita 20, sukari kilo 50, sabuni, vinywaji na unga. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi mahitaji hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti kutoka TFRA Bi.Happness Mbele , amesema Mamlaka ina utaratibu wa kutoa misaada ya aina hiyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii kama taasisi ya serikali.

Alisema kuwa Mamlaka inathamini sana mchango wa wazee hao kwani walipokuwa na nguvu walilitumikia taifa katika nyanja mbalimbali na hivyo kuchangia katika maendeleo ya nchi.

Akizingumza wakati wa kuwakaribisha wageni walio tembelea kituoni hapo, Muuguzi wa Makazi ya Wazee Funga Funga Bi. Reyfrida Ndomba alisena kituo hicho kina jumla ya wazee wapatao 26 wanaopatiwa huduma mbalimbali.

Bw. Hosea Daniel mwakilishi wa wazee hao na mwenyekiti kwa niaba ya wenzake alitoa shukrani za dhati kwa watumishi wa TFRA kwa moyo wa upendo na faraja na kwa muda wao waliojitoa kuwatembelea.

Daniel aliongeza kuwa wazee wanaoishi kituoni hapo wanatambua jitihada za serikali za kuwalea na kuwatunza na kuwalea wazee wasiojiweza na wenye mahitaji maalum.

Post a Comment

Previous Post Next Post