WAKURUGENZI WA RASILIMALI WATU, MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI WAMETAKIWA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA VITENDO VYA RUSHWA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki, Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa yaliyofikia tamati mkoani hapa juzi.
Mkurugenzi  wa Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Batholomea Jungu, akizungumza kwenye ufungaji wa  mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa siku yamwisho ya ufungaji wa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yakifungwa. 

Na Dotto Mwaibale, Singida

SERIKALI  imewataka Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa mikoa kuacha tabia ya kujihusisha na vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali za Umma na kusimamia maadili ya watumishi wa Umma kwa ajili ya kutoa ufanisi wa kazi ili malengo ya serikali yaweze kutimia.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene ameyasema hayo mkoani Singida wakati akifunaga mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki, Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa.

Waziri Simbachewene pia amewataka kwendaKusimiamia majukumu yao kwa weledi na ufanisi na kusimamia maadili ya watumishi ili ufanisi wa kazi uonekene kwa watumishi hao.

Aidha Waziri Simbachawene amewakumbusha majukumu yao mahala pao pa kazi ni kwenda kusimamia taratibu na sheria zilizopo katika maeneo yao.

Akizungumza katika ufugaji wa mafunzo hayo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel alisema, mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza weledi wa utendaji kazi wa Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa.

Baada ya mafunzo haya, baadhi ya washiriki wanasema makosa madogo madogo yaliokuwa yanajitokeza kwenye masuala ya itifaki yatapungua kwa kiasi kikubwa.

Mafunzo haya ya siku mbili ya kuwajengea uwezo kuhusu Itifaki kwenye matukio ya Viongozi wa Kitaifa, kwa Wakurugenzi wa Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa yanafanyika mkoani Singida kufuatia kuwepo kwa changamoto za kiitifaki kwa viongozi hao pale viongozi wa kitaifa wanapotembelea katika maeneo yao. 

Post a Comment

Previous Post Next Post