WAZIRI JAFO-SMT NA SMZ ZIMEDHAMIRIA KUTEKELEZA MIRADI KWA UFANISI

 



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsaidia kubeba ndoo ya maji mkazi wa Sheia ya Banko Jimbo katika Jimbo la Chumbuni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama unaotekelezwa kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo, Januari 4, 2022, Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Shehia ya Banko jimbo la Chumbuni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi wakati kabla ya kuzindua mradi wa maji safi na salama unaotekelezwa kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo, Januari 4, 2022, Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na wananchi baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa Skuli ya Msingi Sebleni Jimbo la Kwahani unaotekelezwa kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo, Januari 4, 2022, Zanzibar.

Mojawapo ya vyumba vya madarasa ya Skuli ya Msingi Sebleni Jimbo la Kwahani yaliyokamilika kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo, Januari 4, 2022, Zanzibar.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMO WA RAIS)

…………………………………………………….

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimedhamiria kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa ufanisi.

Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo Januari 4, 2022 wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kuzindua miradi ya maji safi na salama katika majimbo ya Chumbuni na Amani pamoja ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Skuli ya Msingi Sebleni jimbo la Kwahani yaliyopo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi, inayotekelezwa kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo, Zanzibar.

Akizungumza kwa nyakati tofauti akiwa kwenye ziara hiyo alisema kuwa kupitia usimamizi thabiti wa watendaji Serikali zote mbili zitahakikisha miradi hiyo inakamilika kwa viwango na ufanisi mkubwa.

Pia waziri huyo aliwapongeza wataalamu wanaosimamia miradi hiyo kwa kusema kuwa anafarijika kuona matumizi ya fedha yanaendana na ubora na viwango.

“Leo hii hata ukisema miradi haitekelezeki, mimi nasema hapana maana nimefika hapa na kwa macho yangu nimejionea mwenyewe miradi hii iko vizuri naomba niwapongeze sana kwa kuisimamia vyema na kuitekeleza kwa wakati,” alisema.

Aidha, Waziri Jafo aliongeza kwa kusema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo ya Mfuko wa Jimbo kutaweza kutoa fursa na kuwanufaisha wananchi pamoja na kubadilisha maisha yao kwa ujumla.

Kwa awali akizungumza katika mkutano huo na wananchi wa Shehia ya Banko katika Wilaya ya Magharibi Rashid Simai Msaraka alisema aliahidi kuwa wataendelea kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo zinatumika kama ilivyopangwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Amani, Mhe. Mussa Hassan Mussa alipongeza juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo huku akiwataka kutoiharibu ili iendelee kuwanufaisha.

Post a Comment

Previous Post Next Post